IQNA

Ufunguzi wa maonyesho ya turathi za Kiislamu nchini Russsia

10:29 - February 22, 2009
Habari ID: 1747014
Maonyesho ya turathi za Kiislamu yaliyopewa jina la 'Hazina ya Dunia', yamefunguliwa katika eneo la Jumba la Makumbusho la Kremlin nchini Russia.
Turathi za utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu za tangu zama za utawala wa Ghaznavid na kaumu ya Ghorids huko India na Afghanistan zimewekwa katika maonyesho hayo.
Baadhi ya athari zinazoonyeshwa katika maonyesho hayo ni pamoja na mapambo ya Kihindi ya zama za utawala wa Wamongoli hadi zama za Kiislamu, majambia na panga zilizorembwa mwa madini ya thamani.
Imepangwa kuwa athari zinazoonyeshwa kwenye maonyesho ya turathi za Kiislamu nchini Russia zitahamishiwa katika Jumba la Makumbusho la Armitage kwenye mji wa St. Petersburg.
Maonyesho hayo yanayosimamiwa na Kuwait yamefunguliwa na Waziri wa Habari wa nchi hiyo Swabah Khalid Swabah na maafisa wa Jumba la Makumbusho la Kremlin. 367087

captcha