Kumenukuliwa hadithi za Maimamu Watukufu (as) kuhusu Nairuzi au Nourooz kutoka kwa Imam Swadiq (as) kwamba amesema: “Siku ya Nairuzi ni siku ambayo Mwenyezi Mungu (sw) alifunga agano na mapatano na waje wake kuwa wasimshirikishe na chochote na wawaamini Mitume na warithi wao. Siku ya Nairuzi ni siku ya kwanza ambapo jua lilichomoza. Ni siku ambayo safina ya Nabi Nuh ilifika katika nchi kavi. Siku ya Nairuzi ni siku ambayo Mwenyezi (sw) alimteremsha Jibrail kwa Mtume wake na ni siku ambayo Mtume (saw) alimbeba Imam Ali (AS) kwa mabega yake ili kuteremsha masanamu yaliyokuwa juu ya nyumba ya Mwenyezi Mungu (al Kaaba). Ni siku ambayo Imam Ali (as) aliwashinda maadui wake katika vita vya Nahrwan”.
Katika riwaya nyingine Imam Swadiq (as) anasema: “Wakati inapofika siku ya Nairuzi, oga na vaa nguo bora na safi zaidi na jipake uturi bora zaidi na katika siku hii ni mustahabu kufunga”.
Marejeo: Biharul Anwar, Allamah Majlisi (ma) Juzuu 56. Uk. 61, 62 na 66, Juzuu 57
366565