IQNA

Kituo cha kutayarisha watarjumi wa Qur'ani kuasisiwa

9:52 - February 26, 2009
Habari ID: 1748758
Kwa mara ya kwanza kabisa nchini Iran, kituo maalumu cha lugha cha kutayarisha watarjumi wa Qur'ani Tukufu kitaasisiwa na Taasisi ya Utamaduni ya Tarjuma ya Wahyi katika mji mtakatifu wa Qum.
Kitabu cha Qur'ani Tukufu, yakiwa ni marejeo na chanzo muhimu cha uatafiti wa Kiislamu, tokea wakati wa kuteremshwa kwake karne 14 zilizopita hadi sasa, Waislamu wamekuwa wakikisoma na kukitarjumu kwa makini na kutoa humo masomo na taalumu mbalimbali, kwa kadiri kwamba kitabu hicho kitakatifu ndicho kilichotarjumiwa kwa wingi zaidi uimwenguni. Kitabu hicho kimekuwa kikitarjumiwa na Waislamu na hata wasiokuwa Waislamu kwa malengo tofauti, na mwenendo huo ungali unaendelea.
Moja ya masharti ya kutajumiwa vyema kitabu hiki ni kuwa mtu anayekitarjumi anapasa kuwa mahiri na aliyebobea katika taaluma mbalimbali ili kuweza kuelewa vyema maana hasa ya mambo yaliyomo humo na kuweza kuyabainisha kwa lugha nyepesi na inayofaa kwa manufaa ya watu wengine walio na hamu ya kuelewa maana ya aya za kitabu hicho.
Taasisi ya Utamaduni ya Tarjuma ya Wahyi iliasisiwa mwaka 1995 kwa ushirikiano wa Taasisi ya Wakfu na Masuala ya Kheri ya Wizara ya Utamduni na Muongozo wa Kiislamu. Taasisi hiyo hadi sasa imekwishatarujumi Qur'ani Takatifu katika lugha muhimu 107 za dunia.
Mbali na walimu wa Qur'ani kutoka nchini Iran, kituo hicho maalumu cha kulea watarjumi wa Qur'ani Tukufu pia kitanufaika na walimu mashuhuri wa Qura'ni kutoka nchi nyingine za Ulimwengu. Wanafunzi wa kigeni pia watasajiliwa katika kituo hicho cha kulea watarjumi wa Qur'ani ili kutayarisha watarjumi wazuri watakaoweza kuhudumia vyema kitabu hicho kitakatifu. 369375
captcha