Akizungumzia suala hilo kupitia mahojiano na Kanali ya Nne ya televisheni ya Uingereza, Imos amesema kuwa baraza la mji huo limechukua uamuzi huo kwa lengo la kutangaza mshikamano wake na wakazi wa Ukanda wa Gaza ambao hivi karibuni walikabiliwa na hujuma kali na ya kinyama ya utawala haramu wa Israel.
Ameongeza kuwa kupitia ushirikiano wa mji dada na Ukanda wa Gaza, mji wa Worcester una lengo la kutangaza kuchukizwa kwake na hujuma hiyo ya kinyama iliyotekelezwa na jeshi la utawala haramu wa Israel dhidi ya ukanda huo na kuwaua kwa umati wakazi wake wasio na hatia.
Alan Imos amesema, hatua hiyo pia imelenga kuwaunga mkono wananchi madhlumu wa Palestina, na kuongeza kuwa iwapo itapitishwa na baraza hilo, basi huo utakuwa mji wa kwanza wa Uingereza kuwa na uhusiano kama huo na Ukanda wa Gaza.
Worcester ni mji ulio Kaskazini magharibi mwa London, mji mkuu wa Uingereza. Una jamii ya watu wanaozidi laki tamo. 371457