IQNA

Maonyesho ya sanaa yafanyika mjini Lahore Pakistan

22:21 - March 03, 2009
Habari ID: 1751325
Maonyesho ya sanaa ya wasanii wa Pakistan yatafanyika tarehe 10 hadi 15 mwezi huu wa Machi kwa mnasaba wa kuzaliwa Mtume Muhammad (saw) na Wiki ya Umoja wa Kiislamu katika Kituo cha Utamaduni cha al-Hamraa mjini Lahore.
Kikitangaza habari hiyo, Kituo cha Utamaduni cha Iran katika mji huo kimeeleza kwamba wasanii hao wataonyesha ujuzi wao katika nyanja za uchoraji, hati, sanamu ndogo na uandikaji kwa hati maalumu.
Wasanii hao wa Pakistan wamepata mafunzo katika Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Lahore.
Kituo cha Utamaduni cha al-Hamra ndicho kituo kikubwa zaidi cha utamaduni katika mji huo. 371496
captcha