IQNA

Misikiti iliyoharibiwa ya Malawi kujengwa upya

18:12 - March 04, 2009
Habari ID: 1751878
Rais wa Jamhuri ya Malawi ameunda kamati ya kushughulikia ujenzi wa misikiti 200 iliyoharibiwa na watu wenye misimamo ya kufurutu mipaka ya Kikristo nchini humo yapata miaka kumi iliyopita.
Rais Bingu wa Mutharika amechukua uamuzi wa kujenga upya misikiti hiyo iliyoharibiwa kwa kuchomwa moto na Wakristo wenye misimamo mikali mwaka 1999.
Rais Bingu wa Mutharika amechukua uamuzi huo kwa shabaha ya kuziba ufa uliopo kati ya Waislamu na Wakristo wa Malawi na ametenga bajeti maalumu kwa ajili ya kazi hiyo.
Waislamu wa Malawi wamekaribisha uamuzi huo na kutangaza kwamba kwa sasa kuna idadi ndogo mno ya misikiti nchini humo na kuwa Waislamu wanakabiliwa na matatizo mengi wakati wanapotaka kutumia misikiti hiyo.
Mwaka 1999 waasi wa Kikristo wa kaskazini mwa Malawi walichoma moto misikiti mia mbili ya Waislamu baada ya Muislamu kutoka kusini mwa nchi hiyo kuchaguliwa kwa njia za kidemkrasia kuwa Rais wa nchi hiyo.
Uislamu ni dini ya pili kwa ukumbwa nchini Malawi. Takwimu rasmi zinasema kuwa Waislamu wanaunda asilimia 12 ya jamii ya watu milioni 12 ya Malawi. Hata hivyo Jumuiya ya Kiislamu ya Malawi imetangaza kuwa Waislamu wanaunda asilimia 36. 372558
captcha