Akizungumza jana Jumatano katika kikao cha kimataifa cha 'Uungaji Mkono kwa Palestina, Dhihirisho la Mapambano, Gaza Mhanga wa Jinai' Ali Larijani ameelezea matumaini yake kwamba kikao hicho kitachangia pakubwa katika kutetea na kurejesha haki za taifa shupavu la Palestina.
Sika wa Bunge la Iran amemshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa hotuba yake muhimu aliyotoa katika kikao hicho na kusema kuwa daima amekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za taifa madhlumu la Palestina. Amesisitiza kwamba kutetea taifa la Palestina ni jukumu muhimu linalotokana na thamani za Kiislamu, Kiarabu na kibinadamu. Amesema, taifa la Palestina limepitia machungu mengi yakiwemo ya kufanywa mamilioni ya Wapalestina kuishi kama wakimbizi kwa zaidi ya miaka 60 sasa, wengine wakiwa katika ardhi zao wenyewe, zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
Dakta Larijani amesema ulimwengu mzima hii leo unasubiri kuona mabadiliko halisi katika siasa za mabau za watawala wa Marekani na sio mabadiliko ya kimaonyesho tu na ya hadaa katika siasa hizo. 372913