Mufti Makki pia amelaani maandishi ya gazeti moja la Israel ambalo limetumia maneno ya maskhara kuhusu sira ya Imam Hussein (as). Amekitaja kitendo hicho kuwa ni kiovu na cha kuchukiza.
Amesema kuwa sira ya Imam Hussein ni miongoni mwa sira na historia zenye itibari kubwa mno.
Mufti wa kusini mwa Lebanon amewataka wafuasi wa dini za Kiislamu na Kikristo kuheshimu itikadi na matukufu ya pande hizo mbili na akasisitiza juu ya udharura wa kulinda hali ya maelewano kati ya wafuasi wa dini mbalimbali. 373579