IQNA

Televisheni ya Sahar kutengeneza filamu ya katuni ya vita vya Gaza.

16:05 - March 10, 2009
Habari ID: 1754415
Kanali ya kimataifa ya televisheni ya Sahar imeazimia kutengeneza filamu ya katuni kuhusu vita na mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza.
Mkurugenzi wa televisheni ya kimataifa ya Sahar amesema, katuni mpya ya vita vya siku 22 huko Gaza itakayopewa jina la "Mtoto na Wavamizi" itahusu mapambano ya watoto wa Palestina ya kutetea ardhi yao na kukabiliana na askari wa utawala ghasibu wa Israel.
Maandalizi ya filamu hiyo yanafanyika kwa sasa na itakuwa tayari miezi kadhaa ijayo. 375138

captcha