IQNA

Kongamano la fasihi la "al Mustafa" kufanyika siku chache zijazo

16:08 - March 10, 2009
Habari ID: 1754417
Kongamano la fasihi la al Mustafa linatazamiwa kufanyika tareha 12 mwezi huu wa Machi nchini Iran kujadili maudhui ya nafasi ya mashairi na fasihi katika kueneza na kulingania dini ya Kiislamu.
Mkurugenzi wa kongamano hilo Sayyid Haidar Zaidi amesema kuwa kongamano hilo limetayarishwa na Taasisi ya Kiurdu ya chuo cha Jamiatul Mustafa tawi la Mash'had.
Amesema kuwa hadi sasa makala 30 zilizoandikwa kwa lugha za Kiurdu, Kiingereza, Kiarabu na Kifarsi zimewasilishwa katika sekretarieti ya kongamano hilo.
Makala hizo zinajadili fikra kwamba Mtume hakuwa mshairi, nafasi ya mashairi na fasihi katika kueneza na kulingania dini na nafasi na hadhi ya washairi. 375453
captcha