IQNA

Maadhimisho ya kuzaliwa Mtume (saw) nchini Tunisia

18:37 - March 10, 2009
Habari ID: 1754498
Sherehe za maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Mtukufu (saw) zimefanyika katika msikiti wa Uqba bin Nafi' katika mji wa Qairawan nchini Tunisia.
Wazungumzaji katika sherehe hizo ambazo zilianza kwa usomaji Qur'ani na hotuba ya imam wa msikiti uliotajwa, wamezungumzia masuala mbalimbali yakiwemo ya umoja, usamehevu, kuheshimiana na kukabiliana na watu wenye misimamo ya kupindukia katika dini.
Waziri Mkuu wa Tunisia Muhammad Ghanushi pia ameshiriki katika sherehe hizo ambazo zilipambwa kwa kasida za kuvutia kutoka makundi mbalimbali.
Viongozi wengine walioshiriki katika sherehe hizo ni kutoka matabaka mbalimbali ya serikali, vyama vya siasa, Mufti Mkuu wa Tunisia, wawakilishi wa nchi mbalimbali za Kiislamu na Abdul Aziz at-Tuwaijri, Katibu Mkuu wa Isesco.
Mji wa Qairawan, umechaguliwa kuwa mji mkuu wa utamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu katika mwaka huu wa 2009. 375318
captcha