Kikao hicho kimefanyika kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya, Tiba na Masomo ya Udaktari, Kamati ya Utamaduni na Ustaarabu wa Kiislamu na Iran ( Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiislamu) na Kituo cha Utafiti wa Maadili na Sheria za Udaktari.
Masuala yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni kuhusiana na miongozo ya kitiba katika Uislamu, tiba ya jadi ya Iran, historia ya tiba ya Uislamu na Iran, mustakbali wa kunufaika na urithi wa kitiba na ushirikiano wa mataifa ya Kiislamu katika kuimarisha usalama wa jamii. 375330