IQNA

Ratiba ya Wiki ya Umoja katika Haram ya Imam Ridha (as)

9:54 - March 11, 2009
Habari ID: 1754547
Mkuu wa masuala ya habari na mawasiliano katika Haram ya Imam Ridha (as) huko katika mji mtakatifu wa Mash'had ametangaza ratiba ya sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (saw) na vilevile Wiki ya Umoja wa Kiislamu katika haramu hiyo.
Amesema kuwa ratiba hiyo ilianza kutekelezwa siku ya Jumatatu ambapo mipango mbalimbali ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtukufu Mtume (saw) imekuwa ikitekelezwa katika eneo hilo takatifu.
Wanazuoni na wanafikra mbalimbali wa Kiislamu wamepangiwa kutoa hotuba kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusiana na sifa na maisha ya Mtume na pia kuhusiana na Wiki ya Umoja katika siku hizo za kusherehekea kuzaliwa Mtume Mtukufu (saw).
Ratiba maalumu za kasida za kumsifu Mtume pia zitatekelezwa katika sherehe hizo. Ratiba zote zitakazotekelezwa katika haram hiyo zinaweza kufautiliwa moja kwa moja kupitia anwani ifuatayo: www.razavi.tv. 375967
captcha