IQNA

Jarida maalumu la Itra ya Mtume lasambazwa katika tovuti ya Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu cha Washington

9:58 - March 11, 2009
Habari ID: 1754548
Tovuti ya Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu cha mjini Washington imechapisha jarida maalumu ambalo limepewa jina la Itra ya Mtume Muhammad (saw) kwa mnasaba huu wa kuzaliwa mtukufu huyo.
Jarida hilo linajadili masuala mbalimbali yanayohusiana na maisha, kubaathiwa, malengo ya kupewa utume, majina, lakabu, maadili, tabia na miujiza ya Mtume Muhammad (saw).
Jarida hilo limejadili kwa undani maadili na tabia njema za Mtume Muhammad (saw), jambo lililochangia sana katika kuwafanya watu wakubali kwa haraka dini ya Uislamu.
Pamoja na kuwa inakubalika na wengi kwamba tabia hizo njema za Mtume ndizo zilizochangia kasi ya kuenea Uislamu katika pembe mbalimbali za dunia, lakini maadui wa dini hii tukufu wamekuwa wakieneza propaganda sumu dhidi yake kwa kutoa madai yasiyo na msingi kwamba dini hii inashajiisha utumiaji mabavu katika kufikia malengo yake. 375965
captcha