Muhammad Hussein Sufi, Naibu Mkuu wa Taasisi ya Idhaa na Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB akiwa na wakuu wengine wa taasisi hiyo ameonana na kuzungumza na mamarja' pamoja na wanazuoni mashuhuri wa Kiislamu katika mji mtakatifu wa Qum.
Katika mazungumzo hayo, Ayatullahil Udhma Makarim Shirazi ametoa mkono wa pongezi na fanaka kwa Waislamu wote duniani kwa mnasaba wa kuadhimishwa siku ya kupewa uimamu Imam wa 12 wa Waislamu wa Kishia na vilevile kuadhimishwa Miladu an-Nabi (saw). Amekaribisha ripoti iliyotolewa na wakuu wa taasisi iliyotajwa na kuwataka waendelee na mipango yao ya kuimarisha vipindi vya taasisi hiyo muhimu.
Ayatullah Makarim Shirazi ameashiria ushindi uliopatikana hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza, ambapo wapiganaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas waliweza kuwashinda na kuwafedhehesha askari jeshi wa utawala haramu wa Israel waliokuwa wamejizatiti kwa kila aina ya silaha za kisasa na kusema kuwa, vyombo vya habari vya Iran vilikuwa na nafasi kubwa na muhimu katika ushindi huo. 375898