Kikao hicho kimeandaliwa na Taasisi ya Urithi wa Kiislamu na Kituo cha Utafiti wa Mashariki ya Kati cha Chuo Kikuu cha Cambridge.
Wasimamizi wa kikao hicho wamesema kuwa tayari nuskha 9 muhimu zimewasilishwa kwa kamati inayosimamia kikao hicho na kwamba kati ya hizo kuna mbili za Kiirani. Wanasema kuwa lengo la kufanyika kikao hicho ni kutafiti, kukarabati na kusambaza nuskha kama hizo za kale zilizoandikwa kwa mkono.
Lengo jingine ni kurahisisha upatikanaji wa nuskha hizo na hivyo kuhuisha utamaduni huo wa Kiislamu katika jamii. Akbar Irani mmoja wa wasimamizi wa kikao hicho amesema kuwa lugha mbili za Kiarabu na Kiingereza zitatumika katika utoaji hutuba katika kikao hicho. 376689