Msanii wa Birjand katika mkoa wa Khorasan amekuwa akiandika maandiko madogo kwenye punje za mchele na ufuta. Kwa mujibu wa Iqna kutoka mkoani humo, msanii huyo Sayyid Majid amekuwa akiandika maandishi hayo yakiwemo ya aya za Qur'ani katika punje hizo ndogo, jambo ambalo limewavutia watu wengi.
Msanii huyo amekuwa akifanya uandishi huo kwa muda wa miaka mitano sasa. Pia amekuwa akidhihirisha kipawa chake kikubwa cha usanii katika nyanja iliyotajwa ya uandishi katika matawi ya miti, akitumia pia maji ya dhahabu katika kazi zake hizo.
Msanii huyo amekuwa akishiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ya uandishi wa maandiko hayo madogo. Hivi sasa anajiandaa kushiriki katika tamasha ya kitaifa ya mashindano ya uandishi huo iliyopangwa kufanyika katika mji mtukufu wa Mash'had tarehe 16 mwezi huu. 376714