IQNA

Kitabu cha 'Taamuli katika Qur'ani' chachapishwa nchini Ufaransa

11:31 - March 14, 2009
Habari ID: 1755621
Kitabu kipya cha 'Taamuli katika Qur'ani' kimechapishwa kwa lugha ya Kifaransa nchini humo kwa udhamini wa shirika la uchapishaji la Grasset. Kwa mujibu wa tovuti ya al-Bawaba, kitabu hicho kimeandikwa na Bahjat an-Nadi na Adel Rafat wandishi mashuhuri wa Misri.
Kitabu hicho kinamsaidia msomaji kufahamu sababu za kihistoria na zisizo za kihistoria za kuteremshwa aya za Qur'ani.
Huku wakisisitiza juu ya udharura wa kutarjumiwa vyema na kwa lugha nyepesi aya za Qur'ani, waandishi wa kitabu hicho wanakiri kuwepo kwa matatizo ya kutarjumiwa kwa herufi badala ya maana, kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyomo kwenye kitabu hicho kitakatifu.
Waandishi wa kitabu hicho kilichochapishwa hivi karibuni nchini Ufaransa wanasema kuwa kila mtu anayesoma kwa makini Qur'ani Tukufu, hutambua kwamba kitabu hicho kitakatifu ndicho chanzo bora zaidi cha jibu la kila mielekeo ya kupindukia mipaka na taasubi. Wanasisitiza kwamba Uislamu ni dini ya amani na kwamba haina uhusiano wowote na vitendo vya utumiaji mabavu wa kisiasa. 377454
captcha