Ibada hiyo muhimu itaanza kwa kusomwa Qur'ani saa tano asubuhi na msomaji Qur'ani mashuhuri wa kimataifa Ahad Muhammadi katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Tehran. Baada ya kubainishwa masuala ya kisheria na Hujjatul Islam wal Muslimeen Husseini, kundi la waimbaji kasida la Taha litakaribishwa kuwatumbuiza waumini kwa mnasaba wa kuadhimishwa siku hizi za Maulidi ya Mtume Muhammad (saw).
Hatimaye Mshauri wa Waziri wa Elimu na Malezi ataalikwa kuzungumza na kisha Ayatullah Imami Kashani kuchukua nafasi ya kuwaongoza waumini katika swala ya Ijumaa. 379103