IQNA

Ubora wa athari za Qur'ani katika filamu unategemea ufahamu wa watengenezaji wa filamu hizo

14:37 - March 18, 2009
Habari ID: 1757300
Sekta ya filamu ya Iran inaweza kuwa na ubora wa athari za Qur'ani iwapo tu wanaotengeneza filamu hizo watakuwa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na kitabu hicho kitakatifu.
Hao yamesemwa na Abdu Ridha Akbari, mcheza-filamu mashuhuri wa Iran katika mazungumzo yake na shirika la habari la IQNA. Ameongeza kuwa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, sekta ya filamu ya Iran imekuwa ikizingatia sana masuala ya kimaanawi na kuongeza kuwa licha ya hayo, ubora wa athari za Qur'ani katika sinema na filamu zinazotengenezwa nchini unategemea ufahamu wa watengenezaji wa filamu hizo.
Amesema kuwa tunapozungumzia suala la thamani za kidini katika filamu za Iran hatupasi kuzingatia tu visa vilivyotajwa kwenye Qur'ani bali pia pande nyingine za masuala na mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.
Akijibu swali kwamba, ni kiwango gani cha mafundisho ya dini ambacho mtengenezaji filamu anapasa kuwa nacho ili kutengeneza filamu bora inayozingatia masuala ya dini, Akbari amesema kuwa uelewa wa dhati na wa ndani kuhusiana na mafundisho ya dini wa mtengeneza filamu unaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuboresha filamu kama hizo. Amesema kuwa filamu za Iran zimeweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kutekeleza majukumu yao ya kumuongoza mwanadamu katika njia sahihi ya umaanawi kutokana na kuwa zimeweza kulinda uhusiano mzuri uliopo baini ya watengenezaji filamu hizo na vituo muhimu vya kidini nchini. 379041
captcha