IQNA

Maulana asema, kipindi cha machipuo ni alama ya ufufuo

14:33 - March 18, 2009
Habari ID: 1757302
Katika baadhi ya beti zake za mashairi, Maulana, mshairi mashuhuri wa Iran ambaye ana umaarufu mkubwa katika ngazi za kimataifa anasema kuwa majira ya machipuo ni ishara ya ufufuo katika siku ya Kiama na kufichuka kwa siri za wanadamu.
Hayo yamesemwa na Muhammad Ridha Sangari, mshairi na mtafiti wa fasihi wa Iran ambaye ameongeza kuwa kama ambavyo kipindi cha machipuo ni kipindi cha ardhi kupata sura mpya kufuatia kuchipua kwa mimea kutoka ardhini na miti iliyokauka kupata uhai mpya kutokana na matawi mapya, vivyo hivyo katika siku ya Kiama pia wanadamu watafufuliwa kutoka ardhini baada ya mauti na hivyo kupata uhai na maisha mapya.
Muhammad Ridha Sangari amesema, mwanadamu anapasa kupata somo muhimu kutokana na mabadiliko hayo ya mazingira na kufanya juhudi za kubadilisha mwenendo wake wa maisha kwa maslahi ya maisha yake ya humo duniani na huko Akhera. 379020
captcha