Kwa mujibu wa mtandao wa chuo hicho, nuskha hizo zimechaguliwa kutoka kwenye vitabu 9500vya hati za Kiislamu vilivyoandikwa kwa lugha za Kiarabu, Kifarsi, Kituruki cha Othmania na lugha nyinginezo mashuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu.
Vitabu hivyo vimewekwa katika sekta ya vitabu adimu na maalumu ya maktaba ya Princeton. Lengo la kuwekwa hati hizo katika mtandao ni kuunufaisha umma na thamani kubwa za nakala za maandishi ya zamani zilizoandikwa kwa mkono.
Mpango wa kuwekwa hati hizo kwenye mtandao ulianza kutekelezwa mwaka 2005. Idadi hiyo nzima ya vitabu vilivyotajwa inatazamiwa kuwekwa kwenye mtandao ili kuwanufaisha wasomaji na watafiti, na pia kuwawia rahisi watu wanaotaka kuvinunua.
Michael Cook, mtaalamu wa masuala ya Kiislamu na Asia ya Karibu amevutiwa mno na mpango huo wa Chuo Kikuu cha Princeton na kusema kuwa utawasaidia sana wasomi na watafiti wa nchi za Ulaya na ulimwengu wa Kiislamu.
Nuskha hizo zinazohusiana na vipindi mbalimbali vya historia ya Kiislamu hadi wakati wa kusambaratika utawala wa Othmania zimekusanywa kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu wa Kiislamu, Hispania, Afika Kaskazini, Magharibi, Mashariki ya Kati, India na Indonesia. Zinahusiana pia na masuala na elimu mbalimbali za Kiislamu zikiwemo za historia, falsafa, mantiki, elimu ya kidini (kuhusiana na Qur'ani na Hadithi), sheria, fiqhi, lugha, fasihi, sanaa, sayansi, kemia, unajimu, hesabati, tiba na masuala mengineyo. 379014