IQNA

Uvutiaji katika filamu za kidini na Qur'ani haupasi kupuuzwa

20:36 - March 26, 2009
Habari ID: 1758124
Filamu za kidini na Qur'ani zinatofautiana kidogo na filamu nyinginezo na kwa msingi huo mambo yanayotoa mvuto maalumu katika filamu hizo hayapaswi kupuuzwa. Hayo yamesemwa na Mehran Rajabi, mchezafilamu mashuhuri wa Iran.
Amesema, sekta ya filamu ya Iran imepitia milima na mabonde tokea baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu lakini hata hivyo akasisitiza kwamba jambo ambalo ni muhimu kuzingatiwa hapa ni kuwa filamu zote ambazo zimekuwa zikitengenezwa nchini katika kipindi hiki, zimekuwa zikizingatia maadilii ya Kiislamu ambayo ni thamani muhimu ya kidini na Qur'ani. Amesema, masuala kama vile ya kusema ukweli na uadilifu yamekuwa yakizingatiwa sana katika utengenezaji wa filamu hizo jambo ambalo linakwenda sambamba na misingi ya kidini na thamani za Qur'ani.
Mehran Rajabi ameongeza kuwa mafanikio makubwa ambayo imeyapata Iran katika uwanja wa utengenezaji filamu zinazotilia maanani thamani za dini na Qur'ani, ni kuwa filamu hizo zimepata umashuhuri na kuwavutia watu wengi duniani, na hasa katika ulimwengu wa Kiislamu. Amewashukuru sana viongozi wa serikali kwa kuzingatia uboreshwaji wa filamu hizo nchini na kuongeza kuwa iwapo kuna udhaifu katika uwanja huo, basi unatokana na matatizo ya kifedha na sio irada ya viongozi wa serikali ya kuimarisha sekta hiyo muhimu katika jamii. 380214
captcha