IQNA

Kitabu cha "Nabii wa Mwisho" chazinduliwa Islamabad

11:19 - April 05, 2009
Habari ID: 1760382
Kitabu cha "Nabii wa Mwisho" kimezinduliwa katika sherehe iliyofanyika katika Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Islamabad, Pakistan.
Mwandishi wa kitabu hicho Muhammad Omar Riyadh Abbasi amesema katika sherehe hiyo kwamba sababu ya kuandika kitabu cha Nabii wa Mwisho ni kukabiliana na vitendo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
Mwandishi habari mkongwe wa Pakistan Murtadha Puya ambaye amehudhuria sherehe hiyo amezungumzia nafasi ya kundi potofu la Kikadiani lililoanzishwa na Waingereza sambamba na kuanzishwa kwa kundi la Bahai nchini Iran na lile la Mawahabi huko Saudi Arabia.
Mwishoni mwa sherehe hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Iran mjini Islamabad amesema kuwa hamu ya vijana wa Pakistan ya kutaka kujua marafiki na maadui wao wa kweli ni dalili na mwamko na kuwa macho jamii ya nchi hiyo mbele ya hatari zinazoikabili. 382511
captcha