Mkusanyo wa mashairi ya 'Mimi na Quds Tukufu' ulioandikwa na Suleiman al-Aisi, mshairi mashuhuri wa Syria umechapishwa mjini Damascus, mji mkuu wa nchi hiyo.
Akizungumza na shirika la habari la nchi hiyo, al-Aisi ameashiria umuhimu wa Quds katika historia ya Kiislamu na kuongeza kuwa hii leo eneo hilo tukufu limetajwa kuwa mji mkuu wa utamaduni wa nchi za Kiarabu na kwamba ni wadhifa wa Waislamu wote kufanya juhudi za kutetea na kuwalinda Waislamu wanaoishi katika mji huo, wanaoshambuliwa na kukandamizwa na wavamizi wa Israel. Mkusanyo huo umetimia na kuchapishwa kwa msaada wa Wizara ya Utamaduni ya Syria. Umekusanya mashairi yote yaliyotungwa na al-Aisi kuhusiana na Quds Tukufu na hali ya kusikitisha ya wananchi madhlumu wa Palestina tokea kubuniwa kwa utawala haramu wa Israel katika ardhi zao.
Mashairi hayo yamechapishwa katika kurasa 136 ambapo yanaandamana na picha za Quds na Masjidul Aqsa pamoja na maeneo mengine matakatifu katika ardhi za Palestina. 382985