IQNA

Esesco kuhudhuria kikao cha kimataifa cha Urithi wa Utamaduni nchini Jordan

8:59 - April 06, 2009
Habari ID: 1760791
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni wa Kiislamu la Umoja wa Nchi za Kiislamu Esesco, linashiriki katika kikao cha kimataifa kinachojadili urithi wa kiutamaduni wa Kiislamu mjini Amman Jordan.
Kikao hicho ambacho kilianza siku ya Jumamosi kitaendelea hadi Jumanne tarehe 7 Aprili.
Kikao hicho kinajadili masuala ya urithi, utalii na mabadiliko ya utamaduni katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa bara la Afrika. Kikao hicho kimefunguliwa kwa hotuba ya Waziri wa Utamaduni wa Jordan. 382994
captcha