IQNA

Maeneo ya kidini ya kaskazini mwa Afghanistan kuainishwa

11:59 - April 08, 2009
Habari ID: 1761942
Halmashauri ya Udugu wa Kiislamu ya Afghaistan kwa ushirikiano wa Baraza la Maulamaa wa Kishia na Kisuni la Mkoa wa Balkh imeamua kutuma ujumbe wa kutathmini vituo vya kielimu na kidini, misikiti pamoja na vituo vya masomo ya kidini katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Afghanistan.
Kuhusiana na suala hilo, Maula Abdul Rauf Tawana, Naibu Mkuu wa Halmashauri ya Udugu wa Kiislamu amesema kuwa pamoja na majukumu mengine, ujumbe huo utatembelea misikiti ya swala ya Ijumaa, na hasa msikiti wa Imam Hassan Mujtaba (as) na kufanya mazungumzo na wanafunzi wa Kishia na Kisuni wa masomo ya kidini katika mkoa huo.
Inasemekana kuwa shughuli za kidini zimeongezeka sana katika mkoa wa Balkh katika siku za hivi karibuni na kwa msingi huo juhudi za kuwaunganisha Waislamu zimeimarishwa na wakati huohuo hatua zaidi kuchukuliwa kwa lengo la kukabiliana na watu wenye misimamo ya kupindukia mipaka na wanaozusha ghasia na kutumia mabavu dhidi ya watu wasio na hatia. 384049
captcha