IQNA

Mkutano wa kimataifa wa Anthropolojia katika Utamaduni wa Kiislamu waanza Tunisia

14:05 - April 11, 2009
Habari ID: 1763116
Mkutano wa kimataifa wa Anthropolojia katika Utamaduni wa Kiislamu umeanza kazi zake katika mji wa Qayrawan nchini Tunisia.
Mkutano huo wa siku tatu unahudhuriwa na mtaalamu na mwakilishi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO Muhammad bin Saleh, wasomi wa Kiislamu na wahakiki kutoka nchi za Iran, Tunisia, Algeria, Misri, Syria, Kuwait, Bahrain, Uturuki na Morocco.
Mkutano huo unachunguza anthropolojia (elimu ya binadamu) katika utamaduni wa Kiislamu.
Maudhui nyingine inayojadiliwa katika mkutano huo ni njia za kutumia taaluma ya anthropolojia katika utamaduni wa Kiislamu na kuweka wazi uchunguzi usiokuwa sahihi wa wataalamu wa masuala ya Mashariki wa nchi za Magharibi katika uwanja huo. 385682
captcha