Mtayarishaji wa mchezo huo wa kuigiza Suzan Najmuddin amesema kuwa mchezo huo ni kazi ya kisanii yenye umuhimu mkubwa katika upande wa mtazamo wa kibinadamu. Amewahimiza wasanii wa Syria kufanya juhudi mara dufu za kuwasaidia watoto wa Gaza ambao wanakabiliana na masaibu makubwa.
Suzan Najmuddin amesema kuwa mapato yote yatakayotokana na mchezo huo yatatumwa kwa watoto wa Gaza.
Ameongeza kuwa mchezo huo wa kuigiza ambao ni sehemu ya harakati za misaada ya kibinadmu za kuwaunga mkono wananchi wa Ukanda wa Gaza, utaonyeshwa pia katika nchi kadhaa za kiarabu. 386095