IQNA

Filamu ya Maryam Mtakatifu kuonyeshwa katika televisheni ya Zimbabwe

15:04 - April 13, 2009
Habari ID: 1764334
Filamu ya Maryam Mtakatifu iliyotengenezwa Iran imeanza kuonyeshwa katika televisheni ya taifa ya Zimbabwe.
Filamu hiyo inayoonyeshwa kwa hisani ya Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Harare itarushwa hewani katika sehemu mbili tofauti.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Taasisi ya Utamaduni wa Mawasiliano ya Kiislamu ya Iran imesema kuwa sehemu ya kwanza ya filamu ya Maryam Mtakatifu ilionyeshwa Ijumaa iliyopita sambamba na kuanza sikukuu za Pasaka na sehemu ya pili itarushwa hewani Jumatatu ya leo. Idara hiyo imeishukuru televisheni ya taifa ya Zimbabwe kwa ushirikiano wake mzuri katika kurusha hewani filamu zinazotengenezwa nchini Iran. 386637

captcha