Filamu ya matukio ya kweli (documentary) ya Haki za Binadamu iliyotengenezwa nchini Iran ambayo inahusu manyanyaso yaliyofanywa na Wazayuni dhidi ya kuhani mmoja wa Kiyahudi imefainikiwa kuingia katika fainali ya tamasha ya filamu ya al Jazeera huko Doha, Qatar.
Mtayarishaji wa filamu hiyo Muhammad Ridha Islamlu amesema kuwa filamu ya "Haki za Binadamu" inahusu manyanyaso na mateso ya Wazayuni dhidi ya kuhani mmoja Myahudi na kwamba anatarajia filamu hiyo ya matukio ya kweli itafikisha ujumbe uliokusudiwa. Islamlu amesema kuwa anataraji filamu hiyo itakuwa na mafanikio makubwa katika tamasha ya filamu ya matukio ya kweli al Jazeera huko Doha.
Freedman ni Kuhani wa Kiyahudi ambaye amesimama kupinga Uzayuni bila woga katikati ya bara la Ulaya, suala ambalo limemfanya akabiliwe na vitisho vya kuuawa yeye na familia yake. Islamlu anasema: Kuhani Freedman ambaye amewahi kufanya safari mjini Tehran mara kadhaa na alishiriki katika mkutano wa kimataifa wa Holocaust wa Tehran, anapinga ngano hiyo ya mauaji ya Mayahudi milioni sita katika Vita vya Pili vya Dunia. Jambo hilo limemfanya akabiliwe na unyanyasaji na vitisho vya mauaji vinavyotolewa na Wazayuni wa Israel na barani Ulaya. Kiongozi huyo wa dini ya Kiyahudi ananyanyaswa mno nchini Austria kiasi kwamba hata watoto wake wameshindwa kwenda shule kutokana na vitisho vya mauaji.
Mtengenezaji wa filamu ya Haki za Binadamu anasema familia ya Freedman inaishi katika hali ya kudhulumiwa, vitisho na mashinikizo ya kihoro katika jamii ya Ulaya inayodai kutetea haki za binadamu. 386640