Hayo yamesemwa na Mkuu wa Chuo cha Hadithi cha Tehran Ayatullah Muhammad Muhammadi Reyshahri alipohutubia kikao cha viongozi, wahadhiri na wanafunzi wa chuo hicho na kuongeza kuwa iwapo nguzo hizo nne zitatiliwa maanani katika maisha ya mwanadamu, kiumbe huyo anaweza kufikia maisha timilifu.
Ayatullah Reyshahri amesema kuwa, kutawasali kwa Mwenyezi Mungu kupitia mawalii wake na kufanya juhudi zaidi ni mambo mawili yanayopelekea kujibiwa dua ya mtu.
Amezungumzia umuhimu wa suratul Asr na kusema kuwa sura hiyo ni ratiba kamili ya dunia na akhera ya mwanadamu na kwamba mambo yote yanayomjenga mwanadamu yamekusanywa katika sura hiyo ya Qur'ani. 386284