Kikao cha kimataifa cha Nafasi ya Elimu Katika Uislamu ambacho kimeandaliwa na Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Algeria kitafanyika leo Jumanne na kesho Jumatano huko Algiers, mji mkuu wa nchi hiyo.
Kikao hicho ni sehemu ya shughuli za kituo kilichotajwa cha utamaduni katika kipindi cha mwaka huu wa 2009.
Sheikh Mohamed Lakhal Chourafa Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu wa Algeria ni miongoni mwa watu waliopangiwa kuzungumza katika kikao hicho ambacho kitachunguza kwa kina nafasi ya elimu katika mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu. 387573