Kwa mujibu wa tovuti ya Middle East Online, gazeti hilo limejadili suala hilo katika toleo lake la 90 kwa mnasaba wa siku ya kimataifa ya haki za binadamu.
Baadhi ya maudhui zilizochambuliwa na wataalamu pamoja na watafiti mbalimbali katika katika jarida hilo ni pamoja na Uislamu, dini ya Sheria na ukisasa wa kisiasa, umuhimu wa akili katika Uislamu, Waislamu na serikali ya sheria, Uislamu, haki za binadamu na demokrasia, ukisasa wa Kiislamu na uadilifu, haki za binadamu na mgongano wa staarabu na nafasi ya haki za binadamu katika staarabu mbalimbali.
Katika sehemu nyingine ya jarida hilo, Katayun Amir Pur, mmoja wa wataalamu wa Ujerumani mwenye asili ya Iran amechambua na kuwasilisha utafiti wake kuhusiana na vitabu mbalimbali vinavyomzungumzia Mtume Muhammad (saw) na kusema kuwa katika zama hizi kuna vitabu vingi mno ambavyo vimeandikwa kuhusiana na suala hilo kikiwemo cha Sira ya Muhammad ambacho kimeandikwa na Hans Yansen. 387422