IQNA

Uchunguzi wa athari za Saadi kwa sanaa na fasihi ya Kiirani na Kiislamu

12:42 - April 16, 2009
Habari ID: 1765624
Chuo cha Utamaduni na Sanaa cha Iran kimeandaa kikao cha kuchunguza athari za Mshairi ya Saadi kwa sanaa ya Kiirani na Kiislamu, kwa mnasaba wa kuadhimishwa siku ya kimataifa ya mshairi huyo mashuhuri.
Saadi Shirazi ambaye jina lake halisi ni Abu Muhammad Muslih bin Abdullah ni mshairi mashuhuri kabisa wa nchini Iran na umashuhuri wake umevuka mipaka na kufahamika kote ulimwenguni.
Kitabu chake mashuhuri katika nathari ni Golestan na katika mashairi ni Bustan.
Kikao hicho kimepangwa kufanyika siku ya Jumanne katika ukumbi wa jengo kuu la Chuo cha Utamaduni na Sanaa hapa mjini Tehran. 389130
captcha