Hujjatul Islam Ali Darabi amepongeza hatua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei aliyetangaza mwaka huu kuwa ni mwaka wa Marekebisho ya Mwenendo wa Matumizi na kuongeza kuwa hatua hiyo imechukuliwa kwa lengo la kufikia malengo aali ya Mapinduzi ya Kiislamu.
Sheikh Darabi amesema, mafundisho ya dini ya Kiislamu ni moja ya nguzo muhimu zinazohimiza kujiepusha na ubadhirifu ambako kunaweza kulinda rasilimali za kitaifa kwa ajili ya vizazi vijavyo. Amesisitiza pia juu ya udharura wa kubuniwa mipango ya muda mrefu na kutayarisha mazingira ya kiutamaduni kwa ajili ya kuwaelimisha watoto na tabaka la vijana kuhusu umuhimu wa kujiepusha na ubadhirifu.
Hujjatul Islam Darabi amesisitiza pia juu ya mchango mkubwa wa elimu katika kurekebisha mwenendo wa matumizi ya watu na akasema, taasisi zote za kiutamaduni na elimu zinaweza kutayarisha mazingira mazuri ya kufikia jambo hilo kwa kupanga mikakati mizuri katika uwanaja huo. 388937