Hayo yamesemwa na mwanafikra wa Kiislamu wa Lebanon Muhammad As'ad ambaye ameongeza kuwa mitazamo na fikra za Imam Khomeini zimeacha taathira kubwa duniani hususain katika nchi za Kiislamu kama Lebanon. Amesema kuwa fikra hizo zilipelekea kuboreshwa kwa mwenendo na fikra zisizokuwa za kiadilifu kuhusu vijana, watu maskini na matakabaka ya kati katika jamii za Kiislamu.
Muhammad As'ad amesema kwamba fikra za Imam Khomeini zimesaidia mno katika kuelewa vyema thamani za Kiislamu. Ameashiria pia umuhimu wa mapambano ya Imam Khomeini katika zama hizo na akasema: Itikadi za Kiislamu zilizobainishwa na hayati Imam kwa msingi wa mafundisho ya kidini na Qur'ani zimebadilisha tabia na mwenendo wa Waislamu nwengi.
Mwanafikra huyo wa Lebanon amesema kuwa fikra za Imam Khomeini katika medani ya dini na Qur'ani zimefungua upeo mpya mbele ya vijana wa Kiislamu na kuwasaidia katika kutatua matatizo yao ya kijamii, kiutamaduni, kidini na kiuchumi.
Ameashiria pia nafasi ya muasisi wa Jamhuri ya Kiisalmu ya Iran katika kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiisalmu na akasema kwamba fikra za Imam zimewasaidia Waislamu wa Lebanon katika mapambano yao ya kukabiliana na ubeberu wa Marekani na nchi za Magharibi. 390002