IQNA

8:24 - April 20, 2009
Habari ID: 1767068

Kikao cha 'Amani na Uadilifu katika Vitabu Vitakatifu na Fikra za Kifalsafa' nchini Tunisia

Kikao cha kimataifa cha 'Amani na Uadilifu katika Vitabu Vitakatifu na Fikra za Kifalsafa' kilichoandaliwa na Kituo cha Mazungumzo ya Staarabu na Dini cha Tunisia, kimepangwa kuanza leo Jumatatu katika mji wa Nabil.

Kwa mujibu wa shirika la IQNA, kikao hicho kitawashirikisha wasomi na wanafikra kutoka nchi za Iran, Ufaransa, Misri, Algeria na Morocco.
Kikao hicho cha siku nne kitafanyika katika kamisheni 12 tofauti. Iran itawakilishwa katika kikao hicho na Hujjatul Islam Walmuslimeen Sayyid Abul Hassan Nawwab, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dini na Madhehebu cha mji mtakatifu wa Qum.
Ujumbe wa Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia utasomwa katika kikao hicho. 390877
captcha