Kitabu cha Dini, Utamaduni na Jamiii kilichoandikwa na Hassan Saffar, imam wa msikiti wa mji wa Qatif nchini Saudi Arabia kimeanza kuuzwa katika maduka ya vitabu katika nchi za Saudia na Lebanon.
Kitabu hicho chenye kurasa 736 kinajumuisha hotuba, makala na mahojiano ya mwanazuoni huyo mashuhuri wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Saudi Arabia.
Ayatullah Muhammad Mahdi Asifi ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu ameandika katika utangulizi wa kitabu hicho kwamba ni sehemu ya juhudi za wanazuoni wanaojua vyema changamoto na vitisho vya kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa vinavyowakabili Waislamu na wanaofanya jitihada za kuwaamsha Waislamu mashariki na magharibi mwa dunia. 390883