Kwa mujibu wa gazeti la al-Bayaan la Imarati, shirika hilo limetangaza kwamba miongoni mwa sifa maalumu za kompyuta hiyo ni kasi ya juu ya programu zake na teknolojia ya kisasa kabisa iliyotumika katika mpangilio wa kurasa zake.
Ripoti kuhusiana na suala hilo inasema kuwa, kompyuta hiyo ambayo ina kisomo cha msomaji Qur'ani mashuhuri wa Saudi Arabia Sheikh Abdulrahman as-Sudeis inaongeza kuwa shirika la LG ambalo limeshirikiana na wataalamu kadhaa wa Kiislamu katika kufanikisha mpango huo limeweza kuwaandalia Waislamu mipango mizuri ya Kiislamu na kimalezi. 391443