IQNA

Kun'gara sanaa ya uigizaji ya Iran ni jambo la kusifiwa

15:30 - April 21, 2009
Habari ID: 1768054
Hussein Safarharandi Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesifu kunawiri kwa sanaa ya uigizaji ya Iran katika ngazi za ndani na nje ya mipaka ya nchi na kuwatakia mafanikio zaidi wasanii wanaojishughulisha na suala hilo.
Waziri huyo ameyasema hayo kwa mnasaba wa kuadhimishwa mwezi wa sanaa ya uigizaji nchini pamoja na Siku ya Kimataifa ya Sanaa. Amesema kuwa sanaa hiyo ni muhimu sana kwa taifa la Iran kwa sababu inabainisha, kufahamisha na kudhihirisha utamaduni wa mafundisho ya kijamii na kidini ya Wairani.
Safarharandi amesema kuwa athari za sanaa hiyo ya Iran zimekuwa zikionekana wazi katika ngazi za kimataifa pia, jambo ambalo ni dalili ya mafanikio makubwa ya sanaa ya uigizaji ya Iran. 391574
captcha