Kutokana na juhudi zake za kuimarisha mfungamano wa kiutamaduni na kuhuisha moyo wa jamii mbalimbali za kidini na kiutamaduni kuishi pamoja kwa amani, Umoja wa Mataifa umeamua kuituza Beirut ambao ni mji mkuu wa Lebanon kwa kuutaja kuwa ni Mji Mkuu wa Dunia wa Vitabu katika mwaka huu wa 2009.
Umoja wa Mataifa umetoa taarifa ukisema kuwa umeamua kutunuku na kuishukuru Lebanon kutokana na juhudi zake za kuimarisha moyo wa kuishi pamoja makundi mbalimbali ya kiutamaduni na kidini na kuimarisha mazungumzo kati ya makundi hayo.
Kwa msingi huo sherehe maalumu zimepangwa kufanyika katika ukumbi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, katika mji wa Beirut hapo 25 Aprili ambapo Rais Michel Suleiman Lebanon, Amr Musa, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Abdul Muniim al-Aris, Meya wa mji huo wamealikwa kushiriki.
Shughuli za kupewa mji wa Beirut sifa hiyo ya Mji Mkuu wa Dunia wa Vitabu zitaendelea hadi mwishoni mwa mwaka huu na watu walio na hamu ya kujua zaidi mipango na shughuli hizo wanaweza kutumia anwani ifuatayo: www.beirutworldbookcapital.com.
Beirut ni mji wa pili wa Kiarabu kupewa anwani hiyo. Kuna zaidi ya vituo vya uchapishaji vitabu 360 katika mji huo ambao hadi sasa umeandaa maonyesho mengi ya vitabu. Mji wa Madrid ulipewa anwani hiyo mwaka 2001. Mji wa Alexandria nchini Misri ulifanikiwa kupewa anwani hiyo mwaka 2002. 391839