IQNA

Kufutwa utamaduni, lengo la maadui wa mfumo wa Kiislamu

11:37 - April 22, 2009
Habari ID: 1768308
Akizungumza na Mkuu wa Taasisi ya Televiseni na Redio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mkoa wa Khorasan Kaskazini, Zeinul Abideen Ruhaniniya, Mkuu wa Idara ya Uhubiri wa Kiislamu mkoani humo amesema kuwa lengo kuu la maadui wa mfumo wa Kiislamu wa Iran ni kufuta kabisa utambulisho na utamaduni wa Kiislamu.
Zikisisitiza juu ya umuhimu wa kushirikiana kwa lengo la kuimarisha utamaduni na utambulisho wa Kiislamu, pande mbili hizo zimesema kuwa maadui wa Uislamu hii leo wanaendesha vita vikubwa baridi dhidi ya Uislamu kupitia masuala kama vile ya usekula, thamani za Magharibi na kueneza katika nchi za Kiislamu utamaduni usiofaa wala kuoana na misingi ya mafundisho ya Kiislamu.
Zeinul Abideen Ruhaniniya amesema masuala ya kivutia katika dini yanapaswa kuenezwa na kuwekwa wazi kwa tabaka la vijana kwa kutumia wataalamu waliobobea katika uwanja huo. Huku akisisitiza kwamba shughuli za Qur'ani Tukufu ndio msingi unaofaa wa utamaduni wa Kiislamu, Hujjatul Islam wal Muslimeen Ruhaniniya ameongeza kuwa kuimarishwa kwa utamaduni wa Kiislamu katika jamii kunahitajia uimarishwaji wa mafundisho ya dini. 392215
captcha