IQNA

9:22 - April 26, 2009
Habari ID: 1769588

Kushindwa Marekani katika jangwa ya Tabas ilikuwa kashfa kwa Ikulu ya White House

Khatibu wa sala ya Ijumaa katika mji wa Birjand mashariki mwa Iran amesema kushindwa Marekani huko Tabas kulikuwa pigo kubwa kwa dola hilo lenye kuburi duniani jambo ambalo liliwaibulia kashfa viongozi wa Ikulu ya White House .

Hujjatul Islam Hussein Sadiqi, Imam wa sala ya Ijumaa mjini Birjand ametoa hotuba hiyo kwa munasaba wa tarehe 25 Aprili mwaka wa 1980 ambapo Marekani ilipata pigo kubwa baada ya kushindwa katika njama zake za kuivamia Iran kupitia jangwa la Tabas. Shambulizi hilo lilifeli baada ya tufani ya ajabu kutokea katika jangwa hilo iliyopelekea ndege vamizi za Marekani kugongana angani na hivyo oparesheni hiyo kufeli kwa madhila.
Lengo la uvamizi huo lilikuwa ni kuwanusuru majasusi wa Marekani waliokuwa wakishikiliwa katika pango la majasusi (ubalozi wa zamani wa Marekani) mjini Tehran.
Hujjatul Islam Hussein Sadiqi amesema sababu kuu ya kufeli Marekani katika jangwa la Tabas na katika medani nyinginezo za kijeshi, kiuchumi na kisiasa ni kuwa dola hilo lenye kiburi huzingatia tu masuala ya kidunia katika mahesabu yake na kupuuza masuala ya kimaanawi na kiroho pamoja na mkono wa ghaibu wa Mwenyezi Mungu. 393961

captcha