IQNA

Maktaba ya Jamiatul Mustafa, moja ya mifano michache katika ulimwengu wa Kiislamu

12:37 - April 28, 2009
Habari ID: 1770769
Kwa kuwa na vitabu zaidi ya 90,000 kwenye mtandao wa intaneti, Maktaba ya Jamiatul Mustafa ya Kimataifa, tawi la mji mtakatifu wa Mash'had, ni moja ya mifano michache ya maktaba kama hizo katika ulimwengu wa Kiislamu.
Mfano wa maktaba hiyo ni ile ya Imam Ali (as) ambayo ina vitabu 75,000 lakini bila ya injini ya utafutaji kwenye mtandao. Hayo yamebainishwa na Hujjatl Islam wal Muslimin Hassan Akhlaqi Amiri, Naibu Mkuu wa Jamiatul Mustafa ya Kimataifa anayesimamia masuala ya utafiti katika tawi la taasisi hiyo mjini Mash'had. Amesema kuwepo kwa injini ya utafutaji wa vitabu kupitia mtandao, kunawawezesha watafiti na wanafikra wanaofuatilia masuala mbalimbali ya kielimu kutafuta vitabu tofauti kwa lugha za Kifarsi, Kiingereza na Kiarabu. Ameongeza kuwa kwa kukabiliwa na uchache wa sehemu, hivi sasa wakuu wa taasisi hiyo wanaweza kuwahudumia wanafunzi wa masuala ya kidini na vilevile kuwa na mawasiliano ya kielimu na watafiti mbalimbali kupitia maktaba hiyo.
Huku akisema kuwa maktaba mbili za wanafunzi wa kike na kiume zimeanzishwa katika taasisi hiyo, Hujjatul Islam wal Muslimin Amiri, amesema kuwa maktaba iliyotajwa ya mtandao pamoja na maelezo yanayopatikana humo si jambo rahisi kuonekana katika ulimwengu wa Kiislamu.
Huku akisema kuwa kuna vitabu vya karatasi vipatavyo 12,000 katika maktaba ya wanaume na karibu 6,000 katika maktaba ya wanawake, Hujjatul Islam wal Muslimin Amiri amesema kuwa kwa kuwa na idadi hiyo kubwa ya vitabu, taasisi hiyo inaweza kudai kuwa hakuna maktaba nyingine yoyote iliyo na idadi kama hiyo ya vitabu katika ulimwengu wa Kiislamu. 395537
captcha