IQNA

Makosa ya chapa katika nuskha ya Qur'ani iliyochapishwa Damascus

13:51 - April 28, 2009
Habari ID: 1770772
Waalimu wamegundua kuwepo makosa ya chapa katika nuskha moja ya Qur'ani iliyochapishwa mjini Damscus Syria, huko katika eneo la Jazan nchini Saudi Arabia. Walimu hao Khalid al-Jahni na Muhammad Nahari wa shule ya msingi ya Ahfad katika eneo la Jazan wamesema makosa hayo yalionekana katika baadhi ya sura ambapo jina la Mwenyezi Mungu limefutwa.
Ibrahim Abdou Mu'taba, mkuu wa shule hiyo amesema kuwa makosa hayo ni kufutwa kwa maneno ya Allah, Rabbi, Rabbuhum na Rabbukum katika sura za Qasas, Ankabut, Luqman, Rum na Sajda.
Inasemekana kuwa baada ya makosa hayo kuonekana, wahusika waliiandikia barua Idara ya Wakfu na masuala ya Kiislamu ya Jazan wakiitaka ichukue hatua za dharura za kurekebisha jambo hilo. 395466
captcha