IQNA

12:43 - April 28, 2009
Habari ID: 1770876

Ushirikiano na maelewano ni kati ya njia za kukurubisha madhehebu

Imamu wa Ijumaa wa jamii ya Masuni katika eneo la Birjand mashariki mwa Iran amesisitiza juu ya udharura wa kuwepo umoja na mshikamano miongoni mwa Waislamu.

Katika mkutano wake na Mkurugenzi wa Idara ya Uhubiri wa Kiislamu katika mkoa wa Khorasan Razavi Maulavi Farouqi amesema maelewano na ushirikiano muafaka ni kati ya njia za kukurubisha madhehebu za Kiislamu.
Maulavi Farouqi Imamu wa Ijumaa wa jamii ya Masuni katika mji wa Birjand ameongeza kuwa maelewano ya Waislamu Mashia na Masuni katika mkoa huo ni ya kipekee. Ameongeza kuwa wale wanaozusha mifarakano ni maajenti wa Marekani na mabeberu na kwamba watu kama hawa wanapaswa kuzuiwa kuendesha shughuli zao.
Naye Hujjatul Islam Kadhim Latifian Mkurugenzi wa Idara ya Uhubiri wa Kiislamu katika mkoa wa Khorasan Kusini ambaye pia alihudhuria kikao hicho amesema amani katika mkoa huo imetekana na ushirikiano wa karibu kati ya Masuni na Mashia. 395320


captcha