IQNA

14:42 - April 28, 2009
Habari ID: 1771157

Katibu Mkuu wa OIC ataka kuwepo jopo la kutoa fatuwa

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Ekmeleddin Ihsanoglu amesisitiza juu ya udharura wa kuimarishwa ijtihadi na unyambuzi wa sheria za kifiqhi wa jopo la maulamaa.

Ihsanoglu ameyasema hayo katika mkutano wa kimataifa wa Fiqhi ya Kiislamu unaofanyika mjini Sharja, Imarati
Amesema kuwa Jumuiya ya Kimataifa ya Fiqhi ya Kiislamu ni taasisi marejeo ya kifiqhi na sheria za Kiislamu na inapaswa kufanya jitihada za kuzuia fatuwa za makundi yenye misimamo mikali, suala ambalo pia limesisitwa katika mkutano wa dharura wa viongozi wa nchi za Kiislamu uliofanyika Makka Tukufu.
Katibu Mkuu wa OIC amesema kuwa katika kipindi cha sasa kuna haja kubwa ya kuwepo jopo la maulamaa la kutoa fatuwa na kuzuia fatuwa zinazotolewa na makundi yenye misimamo ya kufurutu mipaka ambazo zimesababisha hasara kubwa kwa ulimwengu wa Kiisalmu.
Karibu wasomi 200 wa Kiislamu wanashiriki katika mkutano huo unaojadili masuala ya kidini, kiuchumi, kitiba na kifikra katika mtazamo wa fiqhi ya Kiislamu. 395346
captcha