IQNA

Uungaji mkono wa Waislamu wa Thailand kwa Wapalestina

14:40 - April 28, 2009
Habari ID: 1771161
Jumuiya ya Waislamu wa Thailand imetangaza uungaji mkono wake kwa wananchi wa Palestina na mapambano yao dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
Jumuiya hiyo imeshonesha vikapu vilivyopambwa kwa nembo inayopinga Uzayuni ambavyo vinauzwa kwa maslahi ya taifa la Palestina.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu wa Thailand amesema kuwa Waislamu wote ni ndugu na wana haki sawa na kwamba jumuiya hiyo imeshonesha vikapu ambavyo mapato ya mauzo yake yatatumwa kwa wananchi wanaokandamizwa wa Palestina.
Amesema vikapu hivyo vina nara inayosema "Simamisheni Mauaji ya Wapalestina." 392730


captcha