Kwa mujibu wa tovuti ya Allafrika, Sheikh Ibrahim Khalil ameyasema hayo alipokutana na mkuu wa Jumuiya ya Wahifadhi wa Qur'ani ya Nigeria na kuongeza kuwa hiyo ni neema kubwa iliyopewa nchi hiyo ya Kiafrika na Mwenyezi Mungu, neema ambayo kwa bahati mbaya amesema haitumiwi vyema wala kuungwa mkono ipaswavyo na viongozi husika.
Sheikh Ibrahim Khalil amewataka Waislamu wote wa Nigeria kuunga mkono na kuwasaidia wahifadhi Qur'ani na kutowazingatia tu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Pia ametoa habari nzuri ya wahifadhi wa Qur'ani kupewa vyeti vya kiwango cha udakta na serikali ya nchi hiyo. 396145